Polisi Monduli wawakumbuka watoto wenye uhitaji maalum

Askari Polisi Wilaya ya Monduli wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wilayani humo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Radegunda Marandu, wametoa msaada wa nguo na vyakula mbalimbali kwa watoto wenye uhitaji maalum wilayani humo.

Msaada huo ulitolewa mapema jana katika Kituo cha Walemavu cha Saint John Paul II Rehabilitation Centre kilichopo wilayani humo ikiwa ni sehemu ya kuihudumia jamii kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Polisi wilayani humo SSP. Radegunda Marandu, alisema kwamba, wamefanya hivyo ili kuliweka kundi hilo karibu hali ambayo itasaidia kushirikishana mambo mbalimbali ikiwemo kupeana taarifa za uhalifu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *