Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Al Maktoum (DWC) Dubai, mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya Kikazi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Februari 6, 2026.
Rais Dkt. Samia alishiriki kwenye Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit – WGS) 2026 pamoja na Uzinduzi wa Jukwaa la Kimataifa wa Uwekezaji Afrika (GAIS).





