Simba Queens, PVB Buyenzi kuvaana

Simba Queens kibaruani Ethiopia | Nipashe

KIKOSI cha Simba Queens kinatarajia kukutana na PVB Buyenzi kutoka Burundi katika mechi ya mwisho ya Kundi B ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa Abebe Bikila jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Tayari Simba Queens ambayo ni vinara wa Kundi B wameshatinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo hivyo wanataka kujua timu itakayoungana na wawakilishi hao wa Tanzania.

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Juma Mgunda, amesema anawapongeza wachezaji wake kwa kuendelea kujituma katika kila mechi na anaamini leo wataendelea kusaka matokeo bora.

“Nina furaha na kuona wachezaji wangu wanaendelea kupambana katika kila mechi, hakuna mechi rahisi, wachezaji wanajituma na wanataka kufikia malengo yetu na ya nchi,” alisema Mgunda.

Wenyeji CBE pia wameshafuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo itachezwa Jumanne wakati fainali itafanyika Agosti 29, mwaka huu

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *