Wednesday, February 18, 2026
spot_img
HomeBiasharaTCDC kinara ubunifu matumizi ya TEHAMA usimamizi wa vyama vya ushirika

TCDC kinara ubunifu matumizi ya TEHAMA usimamizi wa vyama vya ushirika

Katibu Mkuu Kiongozi, Moses Kusilukwa, ameanza kwa kuipongeza Serikali Mtandao pamoja na taasisi mbalimbali kwa juhudi kubwa wanazoendelea kuzifanya katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA nchini, akisisitiza kuwa hatua hiyo imeongeza ufanisi na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Balozi Kusilukwa alitoa pongezi hizo jana Februari 17, 2026 jijini Arusha wakati akizungumza katika Kikao Kazi cha Sita cha Serikali Mtandao (e-Gov), ambapo alieleza kuwa matumizi ya TEHAMA ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali katika kuharakisha maendeleo na kuboresha utendaji wa taasisi za umma.

Alibainisha kuwa TEHAMA imekuwa nguzo muhimu ya mabadiliko ya kiutendaji, ikichochea uwazi, uwajibikaji na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi pamoja na kukuza maendeleo ya watu nchini.

Aidha, aliipongeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa ubunifu na matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU), akieleza kuwa mfumo huo ni mfano bora wa namna TEHAMA inavyoweza kuimarisha usimamizi na uendeshaji wa shughuli za ushirika.

Pongezi hizo zilitolewa wakati Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dk. Benson Ndiege, akiwasilisha maelezo kuhusu mfumo wa MUVU katika banda la maonesho la Tume hiyo ndani ya kikao kazi hicho.

Tume hiyo ni miongoni mwa taasisi zilizotambuliwa kwa matumizi bora ya TEHAMA katika uendeshaji wa shughuli za ushirika, pamoja na kuwa mdhamini wa kikao kazi hicho cha Serikali Mtandao.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments