
ANTONY lazima “apambane” ili kushinda tena nafasi yake katika timu ya Manchester United, kwa mujibu wa kocha Erik ten Hag.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Brazil ni uhamisho wa pili ghali zaidi katika historia ya United baada ya kuwasili kutoka Ajax kwa mkataba wa pauni milioni 82 mwaka 2022.
Lakini amekuwa hana nafasi pale Old Trafford na alicheza kwa dakika moja tu kwenye Ligi Kuu msimu huu.
Hata hivyo, Mholanzi huyo alisisitiza kwamba Antony hatacheza isipokuwa anastahili kupambania nafasi.
“Tutaona itakuwaje,” alisema Ten Hag alipoulizwa kama Antony anaweza kukabidhiwa mwanzo wake wa kwanza wa msimu.
“Tunafanya mazoezi kila siku na wachezaji wanapaswa kupata haki. Mtazamo unapokuwa mzuri na wanaonesha uchezaji mazoezini basi watacheza.”
Luke Shaw anasalia nje ya uwanja kwa sababu ya tatizo la kucheza na kocha huyo amekataa kuweka muda wa kurejea kwa beki huyo wa pembeni.
“Anaendelea vema,” Ten Hag alisema.
“Ni kweli tuna mpango kichwani wakati anaweza kuwa tayari, lakini siku zote unategemea maendeleo yatakwendaje na huwezi kutoa pendekezo kwa sababu kuna mambo mengi, mpango unaweza kuongeza kasi au kupunguza kasi. “