Thursday, February 19, 2026
spot_img
HomeHabariTYDF yakutanisha wadau kuelekea Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania 2026

TYDF yakutanisha wadau kuelekea Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania 2026

Harakati za kuwawezesha vijana nchini zimepata nguvu mpya baada ya wadau wa maendeleo kukutana katika kikao cha nne cha Kamati Tendaji ya Jukwaa la Maendeleo ya Vijana Tanzania (TYDF) 2026, kilichofanyika katika ofisi za Amref Health Africa Tanzania jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kilifunguliwa rasmi na Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dk. Florence Temu, ambaye alisisitiza umuhimu wa kuunganisha nguvu za wadau ili kuhakikisha vijana wanapata fursa, sauti na mazingira bora ya kushiriki katika maendeleo ya taifa.

Majadiliano yaliongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Vijana, Rajabu Suleiman, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DOYODO Tanzania. Alieleza kuwa maandalizi ya TYDF 2026 yanahitaji mshikamano, ubunifu na mikakati madhubuti ili jukwaa hilo liwe jumuishi na lenye matokeo chanya kwa vijana wa kada na maeneo mbalimbali nchini.

Wajumbe wa kamati na wadau wengine walijadili namna bora ya kuimarisha ushirikiano, kuongeza wigo wa ushiriki wa vijana na kufungua fursa zaidi katika sekta za ajira, ubunifu na uongozi. Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha TYDF 2026 inakuwa jukwaa linalosikika, lenye kuwakutanisha vijana na wadau wa maendeleo, na linalochochea mabadiliko ya kijamii na kiuchumi.

Kupitia maandalizi hayo, wadau wanaendelea kuweka msingi imara wa jukwaa lenye sauti ya vijana na mwelekeo wa kuleta matokeo halisi kwa maendeleo ya vijana Tanzania.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments