
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tamko la kutoa wito kwa serikali kutaka uchunguzi huru ufanyike kwa haraka dhidi ya vitendo vya utekaji na mauaji unao endelea sehemu mbalimbali nchini.
Tarifa hiyo iliyotolewa mapema hii leo imeeleza kukithiri kwa vitendo hivyo kuna dhoofisha haki za msingi za watu zinazohakikishwa na katiba ya Tanzania na vitendo hivyo ni kinyume cha demokrasia.
“Marekani inaungana na wale wanaotoa wito wa uchunguzi huru, wa uwazi, na wa haraka kuhusu utekaji unaoendelea na mauaji ya Ali Mohamed Kibao. Mauaji na kupotea kwa watu, pamoja na kukamatwa, kupigwa, na juhudi nyingine za kuwaengua raia katika uchaguzi zilizotokea mwezi uliopita, havipaswi kuwa na nafasi katika demokrasia.
Vitendo hivi vya kikatili vinadhoofisha haki zinazohakikishwa na Katiba ya Tanzania. Tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia ya Bwana Kibao na kwa taifa kwa kupoteza maisha yake na uongozi wake wa kiraia,” imeeleza taarifa ya ubalozi wa Marekani
Sambamba na hilo ubalozi wa Marekani umetoa salamu za rambirambi kwa familia ya Ali Kibao mjumbe wa kamati kuu @chadematzofficial na kutoa pole kwa taifa kwa maisha yake na uongozi wake thabiti kwa chama chake.