Vital’O na ndoto ya kuitoa Yanga Ligi ya Mabingwa Afrika

Kocha Mkuu wa Vital’O ya Burundi, Sahabo Parris amesema kikosi chake bado kina nafasi ya kufanya vizuri dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara Yanga, na kusonga mbele kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Kocha huyo amesema ametumia muda mzuri wa kujiandaa na kikosi chake kwa kusoma makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa mkondo wa kwanza, ambao ulishuhudia wakifungwa mabao 4-0.

Amesema anaamini kwa maandalizi waliyofanya kuna kila dalili za kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kesho Jumamosi Agosti 24, 2024 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

No photo description available.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *