Watu wanne wafariki ajali ya basi la Baraka na Lori Vigwaza

WATU wanne wamefariki dunia akiwemo mtoto mmoja baada ya basi la abiria Kampuni ya Baraka kugongana uso kwa uso na Lori la Mafuta.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema ajali hiyo imetokea maeneo ya Vigwaza baada ya basi hilo lililokuwa likitokea Dodoma kutaka kuyapita magari mengine na kukutana uso kwa uso na lori lililokuwa linaelekwa Rwanda.

Waliofariki katika ajali hiyo ni Wanawake wanne kati yao yupo mtoto mmoja na majeruhi wa ajali hiyo wanatibiwa katika Kituo cha afya Mlandizi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *