Wednesday, February 4, 2026
spot_img
HomeHabariWaziri ataka bodi mpya NEMC iwakazie wanaochafua bahari

Waziri ataka bodi mpya NEMC iwakazie wanaochafua bahari

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yusuf Masauni ameiagiza Bodi mpya ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kushughulikia changamoto ya ukuaji wa haraka wa miji (urbanization) ili kuwe na mipango bora ya matumizi ya ardhi.

Waziri Masauni aliyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akizundua bodi ya tisa ya NEMC itakayoongozwa na Mkuu wa Mkoa mstaafu, Mhandisi Mwanasha Tumbo.

Alisema miji inakua kwa kasi bila mipango bora ya matumizi ya ardhi  hali inayosababisha msongamano, uchafuzi wa mazingira, ukosefu wa mifumo ya maji safi na taka na uharibifu wa vyanzo vya maji na kingo za mito na bahari.

Pia Waziri Masauni aliagiza  bodi hiyo kufanya vikao vyake kama mujibu wa sheria na iweke mikakati madhubuti ya kupata fedha za kujiendesha.

“Nawaagiza mshirikiane kwa karibu na menejimenti ya Baraza ili kuleta matokeo yenye tija na msimamie vizuri Baraza ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira nchini,” alisema.


Aidha, Waziri aliwataka wahamasishe elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira kwani wananchi bado hawana elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira.

Alisema kwa wananchi kukosa elimu ya mazingira kumechangia washiriki katika shughuli zinazochangia uharibifu wa mazingira kama ukataji miti hovyo, uchomaji misitu na utupaji taka ovyo.

“Hakikisheni Baraza linakuwa mamlaka ya usimamizi wa mazingira nchini na linakabiliana ipasavyo na mabadiliko ya tabianchi, kuongezeka kwa joto duniani, kupungua kwa mvua au mvua zisizotabirika, na majanga kama mafuriko au ukame vinachangia kuharibu mazingira na rasilimali za asili,” alisema.


Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Immaculate Semesi alisema baraza hilo limekuwa likifanya uchunguzi utakaosaidia usimamizi na uhifadhi wa mazingira unaofaa na kuratibu utafiti na uchunguzi kwenye mazingira ili kukusanya na kusambaza taarifa kuhusu matokeo ya utafiti na uchunguzi huo.

Alisema NEMC imekuwa ikipitia taarifa ya tathmini ya athari za mazingira na kupendekeza kuhusu utoaji wa idhini ya taarifa za athari kwa mazingira kwa kampuni zinazotekeleza miradi mbalimbali.

Alisema NEMC imekuwa ikibainisha aina ya miradi na programu zinazotakiwa kufanyiwa uhakiki wa mazingira au upelembaji wa mazingira chini ya Sheria  ya EIA na kusimamia udhibiti na utekelezaji wa viwango vya ubora wa mazingira kitaifa.

“NEMC imekuwa ikianzisha na kubuni taratibu na kinga za kuzuia ajali zinazoweza kusababisha uharibifu wa mazingira na pia kubuni hatua za marekebisho pindi zitokeapo ajali pamoja na kuanzisha programu zinazokusudia kuendeleza elimu ya mazingira na elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa usimamizi mwafaka wa mazingira,” alisema


Alisema wamekuwa wakichapisha na kusambaza vitabu vya miongozo, kanuni za kisheria au miongozo kuhusu usimamizi wa mazingira na kuzuia au kupunguza uharibifu wa mazingira.

Alisema NEMC imekuwa ikitoa ushauri wa kitaalamu kwa vyombo vinavyojihusisha na usimamizi wa maliasili na mazingira ili kuviwezeshesha kutekeleza wajibu wake  na kutekeleza kazi nyinginezo zinazotolewa na Waziri anayehusika na mazingira.

Previous article
Benki ya NMB Yadhamini Mkutano Mkuu Maalum wa Jukwaa la Wahariri TanzaniaNa mwandishi wetuBenki ya NMB imeshiriki kikamilifu kama mdhamini wa Mkutano Mkuu Maalum wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika mjini Songea, mkoani Ruvuma. Mkutano huo muhimu kwa ukuaji wa taaluma ya uandishi wa habari nchini, umehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kama mgeni rasmi.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Balozi Dkt. Nchimbi aliwapongeza wahariri na kamati tendaji ya TEF kwa kuandaa uchaguzi wa viongozi kwa kuzingatia misingi ya haki na uhuru, akisema kuwa TEF ni mfano bora wa uongozi wa kikatiba nchini.“Nawapongeza wahariri na kamati tendaji kwa kutambua umuhimu wa kuwa na uchaguzi pamoja na kauli mbiu yenu ya Uchaguzi Huru na wa Haki. Kwa kufanya hivi, mnakuwa mfano wa pekee kwa nchi yetu,” alisema Balozi Dkt. Nchimbi.NMB, ikiwa mdau muhimu wa maendeleo ya sekta ya habari nchini, iliwakilishwa katika mkutano huo na Meneja wa Kanda ya Kusini, Bi. Olipa Habeel. Uwepo wa benki hiyo katika mkutano huo unaonesha dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika kujenga jamii yenye maarifa na uwazi.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, alieleza mafanikio ya jukwaa hilo, likiwemo heshima ya kutoa Rais wa kwanza wa Wahariri Afrika Mashariki.“TEF kwa sasa inatambulika ndani na nje ya nchi kutokana na kazi ya kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari. Heshima ya kuwa na Rais wa kwanza wa Wahariri Afrika Mashariki kutoka Tanzania ni ushahidi wa mchango wetu katika sekta hii,” alisema Balile.Mkutano huo unatarajiwa kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi wapya wa TEF na kujadili mikakati ya kuendeleza taaluma ya habari, licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili wanahabari nchini.Kwa ujumla, ushiriki wa NMB katika mkutano huu ni uthibitisho wa jinsi taasisi hiyo ya kifedha inavyoendelea kujenga mahusiano imara na wadau wa maendeleo, ikiwemo sekta ya habari, ambayo ni mhimili muhimu wa demokrasia na maendeleo ya taifa.
Next article
RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments