Waziri: Wekeni taarifa sahihi kwenye mifumo MaJIS & NISMS

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mwajuma Waziri, ameagiza Watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira (WSSAs) kuweka taarifa sahihi za huduma ya majii na usafi wa mazingira kwenye mifumo ya taarifa ya MaJIS na NISMS, ili kuimarisha ufuatiliaji wa utoaji huduma kwa wananchi.

Akizungumza jijini Dodoma kwenye Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Usafi wa Mazingira lililoratibiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), amesema mifumo hiyo
imekuwa ikiisaidia Wizara, EWURA na wadau wengine kupata takwimu kwa urahisi na haraka.

Aidha, amepongeza EWURA kwa kuwakutanisha wadau wa usafi wa mazingira nchini kwani kupitia kongamano hilo lililofanyika kwa siku mbili, mipango jumuishi ya usafi wa mazingira itawekwa ili kutatua changamoto za milipuko ya magonjwa kama kipindupindu na kusaidia kuwa na jamii yenye afya bora.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *