Sunday, February 8, 2026
spot_img
HomeHabari‎Dk. Samia: Tumejenga upya Kariakoo kulinda ajira, vipato, kuakisi utu

‎Dk. Samia: Tumejenga upya Kariakoo kulinda ajira, vipato, kuakisi utu

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amesema uamuzi wa Serikali kulijenga upya Soko la Kariakoo, umelenga kurejesha vipato, kulinda ajira na kuimarisha hadhi ya biashara, jambo linaloakisi falsafa ya Kazi na Utu.

‎Amesema soko hilo sio la watu au kundi fulani, bali la Watanzania na wasio Watanzania. Pia, amedokeza kuungua kwa Kariakoo kuliangamiza mitaji na kusambaratisha ndoto za matumaini za wafanyabisahara.

‎Dkt Samia ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo, Jumapili Februari 8, 2026 alipofungua Soko la Kariakoo lililojengwa upya baada ya kuungua mwaka 2021.

‎“Ndio maana Serikali imechukua jitihada za kujenga soko upya ili kurejesha kipato, kulinda ajira na kuimarisha hadhi ya biashara ndani ya nchi yetu na huu ndio uhalisia wa Kazi na Utu. Tunapojenga uchumi tunajenga utu wa mtu,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments