
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Mamlaka ya Vitambulisho Vya Taifa (NIDA) Wakala wa Usajili ,Ufilisi na Udhamini( RITA) na Taasisi za uchakataji wa taarifa za waombaji mikopo kwenye Taasisi za Fedha (CREDIT INFO), zimeingia makubaliano ya kubadilishana taarifa kupitia mifumo ya Tehama kwaajili ya kurahisisha ukusanyaji madeni kwa wanufaika wenye kipato.
Hayo yamebainishwa leo, Septemba 11, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk Bill Kiwia katika hafla ya kubadilishana hati za makubaliano kwa taasisi hizo za mkakati na akafafanua kwamba hayo yanafanyika kutokana na maelekezo ya Rais DK Samia Suluhu Hassan.
“Rais Dkt Samia, ameelekeza kwamba hadi kifikia Desemba mwaka huu mifumo yoteya taasisi za Serikali ziwe zinasomana katika mifumo ya kidigitali kwa lengo la kurahisisha utendaji katika kubadilishana taarifa hivyo kwetu tumeanza na hizi na kadri muda unasonga tutakuwa tumekamilisha hili,” amesema.

Ameongeza kuwa kutokana na kukamilisha hilo kwa sasa wataweza kuwafikia wanufaika wa mikopo ya elimu wenye vipato  popote walipo baada ya mifumo kuunganisha na kutoa wito kwa wanufaika ambao hajawalipa mikopo yao waanze kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.
Pia ameongeza kuwa wale ambao bado hawana kipato ni vema wakatafuta njia sahihi ya kuanza kulipa kidogokidogo ili kutoa fursa kwa wanafunzi ambao wapo vyuo kwa sasa waweze kukopa mikopo kwa lengo la kurahisisha michakato ya kupata elimu bila ya changamoto ya kukosa ada na mahitaji mengine.

“Kwa ushirikiano huu wa kubadilishana taarifa kwa njia ya Tehama kwa pamoja tuko tayari kutekeleza majukumu yetu yaliyotufanya tuingie makubaliano haya, hivyo naamini tutawafikia wanufaika wote ambao hajalipa madeni yao popote walipo,†amesema.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Deudedit Buberwa, ametanabaisha kwamba wapo tayari kushirikina katika mfumo huo wa Tehama wa kubadilishana taarifa lengo likiwa ni kupata ufanisi katika upatikanaji wa taarifa zinazohitaka wakati wa kujaza fomu za maombi ya mkopo.

Mtendaji Mkuu ambaye pia ni Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA, Frank Kanyusi, amesema kwamba ili kuhakikisha HESLB, inafanyakazi kwa weledi na watashirikiana nao ipasavyo kwa mujibu ya makubaliano yanavyosema.
“Kupitia mifuko hii ya Tehama ambayo tumeiunganisha na wenzetu Bodi ya Mikopo tutawasilisha taarifa zinazohitajika kuhusu vyeti vya kuzaliwa au cha kifo ikiwa muhusika mzazi au wazazi wake wamefariki.

“Huu ni mchakato wa kawaida kabisa ikiwa mwanafunzi anataka mkopo kutoa taarifa zake zinazohusu cheti chake za kuzaliwa au cha kifo, katika hili tutaendekea kutoa ushirikiano kwa wenzetu wa HESLB kwa mujibu wa makubaliano yetu yanavyosema katika kuthibitisha taarifa zinazohitajika wakati wa kujaza fomu ya maombi ya kupata mkopo,†amesema.
Pia Mtendaji Mkuu wa CREDITINFO, Edwin Urasa, amesema kwamba wao wanafanya kazi na taasisi zote za fedha na wanataarifa zote za wakopaji hivyo wako tayari kufanyakazi na Bodi ya Mikopo kulingana na mahitaji ya makubaliano ya mkataba.

“Natoa rai kwa wakopaji ambao ni wanufaika wa mikopo ya HESLB kuhakikisha wanalipa mikopo kwa mapema ili kutoa fursa kwa wanavyuo ambao wanahitaji kupata mikopo kwa wakati ili kuwaondolea makali ya changamito ya kushindwa kuendekea na masomo mkutokana na kukosa ada.
“Hivyo kwa kuwa tuna taarifa zote za wadaiwa wa mikopo ya HESLB, tunatawafikia popote walipo hivyo wito wetu wajitokeze kulipa bila kuvutana, kwani binafsi ni mnufaika na tayari nimeshalipa, hivyo wengine ambao bado hajawalipa walipe ili Bodi iweze kukopesha wengine ambao wapo vyuoni na wanahitaji mkopo,†amesema.
