Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unatarajia kumpata Rais mpya leo, Oktoba 9, 2026, huku wagombea watatu wakijinadi na kuomba kura za wajumbe wa mkutano maalumu wa uchaguzi unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).
Wagombea hao wanawania nafasi hiyo kupitia uchaguzi unaoshirikisha wajumbe kutoka mabunge ya nchi 184 duniani, huku kila mmoja akitafuta uungwaji mkono wa wajumbe ili kupata ridhaa ya kuongoza taasisi hiyo ya kimataifa inayounganisha mabunge duniani.
Wagombea wa nafasi hiyo ni Milton Dick kutoka Australia, Profesa Dkt. Sahiba Gafarova kutoka Azerbaijan na Rojo Edwards kutoka Chile.
Atakayeshinda uchaguzi huo atamrithi Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, ambaye amekuwa Rais wa IPU tangu mwaka 2023.
#IPU153Tanzania








