HomeAfyaMUHAS yahamasisha mazoezi kukabili magonjwa yasiyoambukiza

MUHAS yahamasisha mazoezi kukabili magonjwa yasiyoambukiza

Wananchi wametakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara, kuzingatia lishe bora na kufuatilia afya zao ili kupunguza hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukiza, ambayo yanaendelea kuwa changamoto ya kiafya nchini.‎‎

Wito huo umetolewa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), kikisisitiza umuhimu wa elimu na uhamasishaji katika kujenga uelewa wa jamii kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa hayo.‎‎

Katika kuendeleza juhudi hizo, MUHAS imeandaa matembezi na mbio za hisani kwa msimu wa tano, zilizofanyika katika kampasi ya chuo hicho na kushirikisha zaidi ya watu 700, wakiwemo wahitimu, wanafunzi, wafanyakazi na wadau wa afya kutoka ndani na nje ya nchi.‎‎

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Bruno Sunguye, amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi, kuzingatia ulaji bora na kufahamu hali zao za kiafya ili kupunguza hatari ya magonjwa yasiyoambukiza.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments