HomeHabariIPU yataka matumizi AI kudhibiti upotoshaji taarifa

IPU yataka matumizi AI kudhibiti upotoshaji taarifa

Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) umeazimia kuwepo kwa mifumo ya kudhibiti matumizi ya akili unde (AI) na teknolojia za kidijitali ili kudhibiti upotoshaji wa taarifa, usalama wa taarifa na haki za binadamu.

Pia, umeazimia akili unde itumike katika kuimarisha ushiriki wa wananchi kwenye uamuzi wa umma, huku yakisisitiza kuwepo kwa mifumo ya udhibiti.

Pendekezo hilo, ni miongoni mwa maeneo matano ya utekelezaji yaliyoainishwa katika Tamko la Arusha (Arusha Communiqué), lililowasilishwa wakati wa kuhitimishwa kwa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), jijini Arusha.

Tamko hilo, lilisomwa kwa pamoja na Mwenyekiti Wabunge wa Tanzania IPU na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya IPU kutoka Bangladesh, Barrister Jahrat Adib Chowdhury.

Limezitaka nchi kuangalia namna teknolojia mpya zinavyoweza kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kuwapa wananchi nafasi zaidi ya kushiriki katika shughuli za kibunge.

#IPU153Tanzania

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments