
ufunguzi wa mashindano ya Ndondo Cup Dodoma kwa mchezaji wa Nkuhungu Terminal FC, Kassim Hussein,
baada ya mechi dhidi ya Kikuyu FC iliyopigwa jijini humo juzi.
MICHUANO ya Ndondo Cup 2024, inaendelea jijini Dodoma baada ya kuanza mwishoni mwa wiki, huku ikiangazia dhamira thabiti ya Serikali ya Marekani ya kuunganisha michezo na mipango muhimu ya afya inayolenga kupambana na VVU na kukuza chanjo miongoni mwa vijana wa Tanzania.
Katika mpango huo ambao unaongozwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Ukimwi (PEPFAR) kupitia mradi wa Breakthrough ACTION, unaifanya michuano hiyo ya soka ya ngazi ya chini kuvuka mipaka ya matukio ya jadi ya michezo, yakitumika kama jukwaa lenye nguvu la elimu ya afya na ushirikishwaji wa jamii.
Kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana kutoka kwa matukio ya awali ya Ndondo Cup yaliyofanyika Dar es Salaam, Iringa, Mbeya, Mwanza na Ruvuma – ambapo makumi ya maelfu walipata huduma muhimu za afya – mashindano ya mwaka huu yanalenga kuongeza ushawishi wake kupitia kampeni ya vijana ya ‘Sitetereki’ na mpango wa chanjo wa ‘Kuwa Bingwa’.
Mwakilishi wa USAID, Moses Bateganya, alisisitiza ushirikiano kati ya michezo na afya kwa kueleza: “Tumejizatiti kuanzisha mbinu za ubunifu zinazotoa matokeo halisi ya afya. Tunaamini michezo inaweza kuwa nguvu kubwa katika kuleta na kukuza mabadiliko chanya ya tabia na kuboresha upatikanaji wa huduma, na tunafurahi kushirikiana na Ndondo Cup na Serikali ya Tanzania kuleta mpango huu katika uhalisia.â€
Evangelina Chihoma kutoka Mfuko wa PEPFAR, yeye alisisitiza umuhimu wa kuwafikia vijana, akiangazia takwimu za utafiti uliofanyika hivi karibuni ukionesha kuna haja kubwa ya kufikia vijana na elimu ya huduma za VVU.
“Mfuko wa PEPFAR unaendelea kujizatiti kupambana na VVU Tanzania†alisema. “Lengo letu ni kufikia vijana kwa njia mablimbali za kibunifu kama Kombe la Ndondoâ€.
Kampeni ya ‘Sitetereki’ inalenga hasa vijana wenye umri wa miaka 15-24, ikiwawezesha kuchukua jukumu la afya zao. Washiriki wanaweza kupata taarifa muhimu kuhusu VVU, kupima, kupata kinga kabla ya maambukizi (PrEP), tiba ya kufubaza virusi vya ukimwi yaani antiretroviral (ART), iwapo wamepimwa na kupatikana na VVU, yote haya wakifurahia msisimuko wa michuano hiyo.
Wakati huo huo, mpango wa ‘Kuwa Bingwa’ unahimiza wanaume kuweka kipaumbele kwenye chanjo, huku huduma za chanjo zikifikika kwa urahisi kwenye uwanja wa michezo, zikiimarisha umuhimu wa afya kwao na familia zao.