Ndoa ya Dabo na Azam imevunjika

Klabu ya Azam FC imetangaza rasmi kuachana na kocha Youssouph Dabo na kuvunja benchi la ufundi la timu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Azam FC leo Septemba 3, 2024 inaeleza kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili.

“Bodi ya wakurugenzi ya Azam FC na kocha, Youssouph Dabo, wamefikia makubaliano ya pande mbili ya kutoendelea kufanya kazi pamoja kuanzia leo, Septemba 3, 2024.

“Dabo aliyehudumu kwenye klabu hii kwa kipindi cha mwaka mmoja, anaondoka na wasaidizi wake wa benchi la ufundi aliokuja nao.

“Klabu pamoja na wadau wake inapenda kumshukuru Dabo kwa weledi na moyo wake wa kutokata tamaa katika kipindi chote alichokuwa nasi na tunamtakia kila la kheri huko aendako.

“Aidha, wakati bodi ikiwa kwenye mchakato wa kutafuta kocha mpya, programu za timu zitakuwa chini ya makocha wa timu zetu za vijana,” ilifafanua taarifa hiyo ya Azam FC.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *