
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Million 30 kwa ajili ya Timu Taifa ya Wasichana ‘Serengeti Girls’, baada ya kutwaa Ubingwa wa UNAF U-17 fainali zilizofanyika Tunisia 2024.
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Damas Ndumbaro amewakabidhi fedha hizo wachezaji hao kwenye Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ( TFF)



