Shule Dodoma zaanza kuunga mkonoMatumzi nishati safi ya kupikia

BAADHI ya wamiliki wa shule mkoani Dodoma wameunga mkono wito wa Rais Samia Suluhu Hassan wa matumizi ya Nishati safi shuleni, wakisifu na kueleza ni hatua ya kuelekea katika mwelekeo sahihi.

Mmiliki na Mwanzilishi wa Shule za Elshaddai mkoani humo, Juliana Kalinga anasema mabadiliko hayo ya nishati safi katika taasisi hiyo yamesaidia kupunguza gharama zisizo za lazima hivyo kuokoa matumizi makubwa.

Akizungumza mkoani huko alipotembelea shuleni kwake, juliana ambaye pia ni Ofisa wa Chama cha Wamiliki wa Shule Wanawake Tanzania (TAWOSCO) alisema taasisi zinazoendelea kutumia mkaa na kuni zinapaswa kuhama haraka na kutumia nishati safi ili kuongeza ufanisi.

“Kuna faida nyingi za kutumia nishati safi ambazo ni pamoja na kuwalinda wafanyakazi wetu dhidi ya moshi unaosababisha matatizo ya kupumua, mazingira machafu ya kazi, ulinzi wa miti yetu miongoni mwa mambo mengine” anasema Juliana

Juliana anasema Shule yake ni miongoni mwa shule za kwanza kuanzisha matumizi ya nishati safi katika mkoa huo akisistiza hajawahi kujutia kutumia nishati hiyo.

“Wanafunzi wangu wanakula kwa wakati, wafanyakazi wanabaki safi kwa sababu hawahangaiki na moshi au mazingira machafu. wakati wa msimu wa mvua tuko salama kwa sababu hatuhitaji kushughulika na kuni zenye mvua” anasema juliana

Shule ya Elshaddai ina wanafunzi 1000, na kila mwezi, juliana anasema huhakikisha anaweka LPG kuhakikisha kuwa makaa na kuni hazipati nafasi.

Meneja wa Masuala ya Shirika la Taifa Gesi Angelllah Bhoke, anasema wao wanafanya kazi kuhakikisha kila gesi inapopungua inapatikana na kwmaba hicho ndicho wanachokifanya kwa taaisis nyingine zote kwa sababu ana miundombinu imara ya usafiri inayo hakikisha hakuna mteja atakayekosa.

Rais Samia Suluhu Hassan kwa sasa anaongoza ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia katika kufanikisha hilo tayari ameshaagiza taasisi zote zinazohudumia wanafunzi zaidi ya 100 ziingie katika mfumo huo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *