Mgombea Ubunge wa Ukonga kupitia CCM, Jerry Silaa, amemnadi na kumuombea kura Mgombea Udiwani wa Kata ya Zingiziwa, Selemani Kanniki, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Septemba 20, 2025 eneo la Lubakaya.
Silaa aliwataka wananchi wa kata hiyo kumchagua Kanniki pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan na yeye mwenyewe ili kushirikiana kuwaletea maendeleo, ikiwemo ujenzi wa barabara kilometa 72.




Kwa upande wake, Kanniki alisema Zingiziwa imenufaika na miradi mingi ya maendeleo ndani ya miaka minne na akaomba serikali kuendeleza jitihada hizo kwa barabara za kiwango cha lami katika maeneo mbalimbali.
Aidha, aliwataka viongozi wa shule kuepuka michango isiyo na tija kwa wanafunzi, hasa ya chakula.





