Monday, April 20, 2026
spot_img
HomeMichezoMouine Chaabani: Kocha Bora Afrika aendelea kung’ara

Mouine Chaabani: Kocha Bora Afrika aendelea kung’ara

Huyu hapa ni Mouine Chaabani, kocha raia wa Tunisia ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa klabu ya RS Berkane. Chaabani anatajwa kuwa miongoni mwa makocha wa Kiafrika walio na mafanikio makubwa katika miaka ya karibuni.

‎Umaarufu wake ulianza kupanda kwa kasi mwaka 2018 alipoiwezesha Espérance Sportive de Tunis kutwaa ubingwa wa CAF Champions League, kabla ya kurudia mafanikio hayo mwaka 2019 kwa kutwaa tena taji hilo.

‎Katika miaka iliyofuata, Chaabani aliendelea kuonyesha ushindani mkubwa barani Afrika, akifikia hatua ya robo fainali mwaka 2020 na nusu fainali mwaka 2021 akiwa bado na Espérance.

‎Mwaka 2022, akiwa na Al Masry SC, aliishia robo fainali ya CAF Confederation Cup. Baadaye alijiunga na RS Berkane ambapo aliifikisha fainali ya mashindano hayo mwaka 2024, kabla ya kutwaa ubingwa mwaka 2025.

‎Katika msimu wa sasa, ameiongoza RS Berkane kufika nusu fainali ya CAF Champions League, akiendelea kuthibitisha uwezo wake mkubwa katika soka la Afrika.

‎Kwa mafanikio hayo, Mouine Chaabani anaendelea kujijengea heshima kama mmoja wa makocha bora zaidi barani Afrika kwa sasa, akiwa mfano wa makocha wanaoonyesha ubora, uthabiti na ushindani wa hali ya juu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments