Mrembo Latricia Ian ametangazwa mshindi wa Miss World Tanzania 2026, akiwakilisha Dar es Salaam (Ubungo), na sasa anatarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World kimataifa.
Latricia anajivunia kuunganisha urembo na dhamira ya kijamii kupitia mradi wake wa Nuru ya Elimu, unaolenga kuwawezesha vijana kwa kuwapatia fursa za elimu.
Kitaaluma, ni mtaalamu wa mawasiliano na uongozi, akifanya kazi kama Client Manager Studio za Infocus, ambako amejijengea uzoefu mkubwa katika mawasiliano ya kimkakati na uongozi.
Anaamini kuwa urembo wa kweli huonekana kupitia huduma kwa jamii na matumizi sahihi ya sauti yako kuleta mabadiliko chanya.
Katika matokeo hayo, Nouru Masoud alishika nafasi ya mshindi wa pili (1st Runner-Up), akifuatiwa na Paulina Allute (2nd Runner-Up), Silya Mussa (3rd Runner-Up) na Dian Rutagalinda (4th Runner-Up).





