Monday, May 25, 2026
spot_img
HomeHabariAginatha Rutazaa aomba mahakama maalum kushughulikia ukatili wa kijinsia

Aginatha Rutazaa aomba mahakama maalum kushughulikia ukatili wa kijinsia

MWANAHARAKATI nguli nchini, Aginatha Rutazaa, ameiomba serikali kuunda Mahakama Maalum, itakayokuwa na jukumu la kushughulikia kesi pekee zinazohusu ukatili wa kijinsia.

Rutazaa, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TUSONGE CDO, amesema kesi hizo kwa sasa zinashughulikiwa katika mahakama za kawaida na mara nyingi hazipati ule uzito wake wa kufanyiwa kazi kwa haraka, kwa ajili ya kusaidia wale waathirika waliofanyiwa matukio hayo.

Alikuwa akizungumzia leo, Desemba 2,2024  siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza Novemba 25 na zikitarajiwa kufikia ukomo wake Desemba 10 mwaka huu.

“Tunajua kesi hizi zinashughulikiwa katika mahakama za kawaida na mara nyingi hazipati ule uzito wake wa kufanyiwa kazi kwa haraka kwa ajili ya kusaidia wale wahanga  waliofanyiwa matukio haya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments