HomeMichezoBocco, Mkude kuagwa mbele ya mashabiki Simba Day

Bocco, Mkude kuagwa mbele ya mashabiki Simba Day

Klabu ya Simba SC imetangaza kuwa itawaaga rasmi manahodha wake wa zamani, John Bocco na Gerard Mkude, wakati wa Tamasha la Simba Day litakalofanyika Septemba 10, 2026, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema uamuzi huo umetokana na mchango mkubwa walioutoa wachezaji hao katika mafanikio ya klabu kwa miaka mingi.

“John Bocco na Gerard Mkude ni sehemu ya historia ya Simba. Wameitumikia klabu kwa uadilifu, kujituma na uzalendo mkubwa, na wamechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio yetu ndani na nje ya nchi,” amesema Ahmed.

Ameeleza kuwa uongozi wa Simba tayari umezungumza na Bocco na Mkude, ambao wamekubali kushiriki tamasha hilo ili kupewa heshima na kuagwa rasmi mbele ya mashabiki na wadau wa soka.

Bocco aliiongoza Simba kutwaa mataji kadhaa ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, huku Mkude akiwa mmoja wa viungo waliodumu kwa muda mrefu na kutoa mchango mkubwa katika mafanikio ya klabu.

Mbali na kuwaaga nyota hao, Simba Day pia itatumika kutambulisha kikosi kitakachoivaa klabu hiyo katika msimu wa 2026/27.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments