HomeBiasharaTAFFA kuanzisha mfumo mpya wa forodha kielektroniki kuanza Agosti 1

TAFFA kuanzisha mfumo mpya wa forodha kielektroniki kuanza Agosti 1

Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) kimetangaza kuanza kutumika kwa mfumo mpya wa kielektroniki wa kurahisisha shughuli za uingizaji na usafirishaji wa bidhaa kuanzia Agosti 1, 2026.

Mfumo huo umeunganishwa na Tanzania Electronic Single Window (TANESW) kwa lengo la kuongeza ufanisi, uwazi na kurahisisha utoaji wa huduma za uwakala wa forodha kwa njia ya kielektroniki.
‎
‎TAFFA imesema mfumo huo utatumika katika uingizaji wa bidhaa nchini, usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi pamoja na mizigo ya transit inayopita Tanzania Bara kuelekea nchi jirani, isipokuwa bidhaa au huduma zilizosamehewa chini ya GN Na. 83 ya mwaka 2026.
‎
‎Utekelezaji utaanza kwa awamu ya majaribio kwa kushirikisha baadhi ya kampuni za uwakala wa forodha kabla ya mfumo huo kuanza kutumika rasmi kwa wadau wote.
‎
‎TAFFA imewataka wanachama na wadau wa biashara kujiandaa mapema kwa matumizi ya mfumo huo na kufuatilia taarifa rasmi kuhusu usajili, mafunzo na taratibu za matumizi kupitia njia rasmi za chama.
‎

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments