HomeMichezoKamwe: Abuya aumia nyama za paja katika Dabi ya Kariakoo

Kamwe: Abuya aumia nyama za paja katika Dabi ya Kariakoo

Kiungo wa Yanga, Duke Abuya, amepata jeraha la nyama za paja baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa Simba, Libasse Gueye, katika Dabi ya Kariakoo iliyomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe, amesema taarifa ya awali ya daktari wa klabu hiyo, Moses Etutu, inaeleza kuwa Abuya ameumia nyama za paja, hali iliyomlazimu kushindwa kuendelea na mchezo huo.

Pambano hilo limechezwa katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, huku jeraha hilo likiwa pigo kwa Yanga baada ya kiungo huyo kushindwa kumalizia mchezo dhidi ya watani wao wa jadi.

Kupitia ujumbe wake, Yanga imemtakia Abuya nafuu ya haraka kwa kutumia maneno, “Get Well Soon General,” huku akisubiriwa kufanyiwa tathmini zaidi ya kitabibu ili kubaini ukubwa wa jeraha hilo na muda anaoweza kukaa nje ya uwanja.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments