HomeBiasharaKibiti: Mkurugenzi akamata gari lililosafirisha mchanga bila risiti

Kibiti: Mkurugenzi akamata gari lililosafirisha mchanga bila risiti

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Ramadhan Kimara, amekamata gari lililokuwa likisafirisha mchanga kutoka kwenye shimo la mchanga bila kuwa na risiti ya malipo ya ushuru.

Kimara amekamata gari hilo Octoba 14 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa vyanzo vya mapato katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Katika ukaguzi huo, Kimara amefuatilia namna watendaji wenye dhamana ya ukusanyaji mapato wanavyotekeleza majukumu yao, na kuhakikisha malipo yanafanyika kwa taratibu zilizowekwa na kurekodiwa katika mfumo rasmi wa ukusanyaji.

Mkurugenzi huyo amesema ukaguzi huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha usimamizi wa mapato ya Halmashauri na uwajibikaji wa watendaji, ili fedha zinazokusanywa zichangie utoaji wa huduma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi wa Kibiti.

Mwanzoni mwa wiki hii Mkurugenzi Kimara alikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mkupuka iliyopo Kijiji cha Mkupuka ambayo inatarajiwa kugharimu Sh.milioni 528.

Akiwa katika eneo la mradi, alizungumza na fundi pamoja na msimamizi wa ghala la vifaa vya ujenzi, na kuwapa maelekezo ya kuhakikisha vifaa vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa, huku akimtaka fundi kukamilisha kazi ndani ya muda wa mkataba.

Aidha Kimara alimtaka Mhandisi wa mradi kutembelea eneo la ujenzi mara kwa mara ili kufuatilia maendeleo ya kazi na kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza na kuchelewesha mradi huo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments