HomeElimuMbunge Mgonto afundisha hisabati mashuleni

Mbunge Mgonto afundisha hisabati mashuleni

Mbunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki, Thomas Mgonto, ameendelea na kampeni yake ya kutembelea shule za sekondari zilizopo katika jimbo lake kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi, hususan Hisabati, ambayo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto mbalimbali katika ufaulu.

Katika utekelezaji wa mpango huo ambao ameupa jina la Sikonga Mtaa kwa Mtaa na Chifu Mgonto, amekuwa akiingia moja kwa moja darasani na kufundisha somo la Hisabati kwa wanafunzi wa Kidato cha Pili na Kidato cha Nne, huku akitumia nafasi hiyo kuwahamasisha wanafunzi kujenga msingi imara katika masomo hayo muhimu kwa maendeleo yao ya kitaaluma.

Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada zake za kutafuta namna ya kuongeza hamasa kwa wanafunzi katika kujifunza Hisabati na masomo mengine ya sayansi, ambayo yana umuhimu mkubwa katika kuwaandaa vijana kupata taaluma mbalimbali zinazohitaji ujuzi wa kisayansi na kiteknolojia.

Shule ambazo amezitembea na kufundisha wanafunzi ni shule ya sekondari Siuyu, Lighwa, Dung’unyi seminari, Ntuntu,Munghaa, Munkinya,Mkiwa,Mtaturu na Unyahati sekondari.

Mbunge huyo katika ziara zake kwenye shule hizo amekuwa akiwataka wanafunzi kuwa na nidhamu, kuhudhuria masomo kwa wakati na kutumia muda wao mwingi katika kujisomea na kufanya mazoezi ya Hisabati pamoja na masomo mengine ya sayansi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments