WATU watatu wamefariki dunia, akiwemo mtoto wa miezi mitatu, baada ya meli ya MV Chambo kuteketea kwa moto alfajiri ya leo, Jumapili, Oktoba 11, 2026, katika Ziwa Nyasa, Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Peres Magiri, amesema katika taarifa za awali kwa njia ya simu kuwa meli hiyo ilikuwa na abiria 44 na ilikuwa ikisafiri kutoka Bandari ya Mbamba Bay, Tanzania, kuelekea Msumbiji.
Amesema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, huku uchunguzi kuhusu tukio hilo ukiendelea.




