Tuesday, March 3, 2026
spot_img
HomeHabariTanzania yatoa majibu ya hatua zake kuhusu Uchaguzi Mkuu Baraza la Haki...

Tanzania yatoa majibu ya hatua zake kuhusu Uchaguzi Mkuu Baraza la Haki za Binadamu

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa majibu ya hatua zilizochukuliwa katika kulinda amani na wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu Oktoba 2025 kwa Baraza la Haki za Binadamu huku ikisisitiza kuwa zilikuwa ndani ya jukumu lake kulingana na sheria za nchi.

Akizungumza katika kikao cha 61 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika Geneva Machi 2 2026, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) Mjini Geneva, Dk.Abdallah Possi, amesema serikali imesikitishwa na kauli zilizotolewa na baadhi ya washirika wa kimataifa pamoja na mashirika ya haki za binadamu kuhusu matukio yaliyohusishwa na Uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

Amesema Tanzania kama nchi huru ina wajibu wa msingi wa kulinda amani ya umma, mfumo wa kikatiba na usalama wa wananchi wake na kwamba hatua zilizochukuliwa na Serikali zililenga kuzuia vurugu, kulinda amani na kudumisha utulivu wa nchi kwa mujibu wa sheria za nchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments