Monday, April 20, 2026
spot_img
HomeAfyaWadau waombwa kushiriki Mkunga Half Marathon

Wadau waombwa kushiriki Mkunga Half Marathon

Wakunga wameomba wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kushiriki Mbio za Mkunga Half Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Mei 2 mwaka huu, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Ombi hilo limetolewa na Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Dk.Beatrice Mwilike, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Amesema Mbio hizo zinatarajiwa kuwa na washiriki 2000, na kwamba wakijitokeza wadau wengine zaidi ni vizuri.

Amesema mbio hizo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo kilele chake ni Mei 5 ya kila mwaka, ambapo safari wameamua kuadhimisha kwa njia hiyo.

Kama watajitokeza watu wengine zaidi, itapendeza, ila ninachowaomba, ni kwamba waendelee kujisajili kwa ajili ya kushiriki mbio hizi zilizoandaliwa na TAMA, Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ” amesema.

Amefafanua kuwa katika mbio hizo, wanatarajia kukusanya rasilimali kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ya uzazi, kwa lengo la kufikia Sh.bilioni moja.

“Maadhimisho ya mwaka huu pia yanalenga kuongeza uelewa wa Jamii kuhusu nafasi muhimu ya Wakunga katika kuhakikisha uzazi salama, kutoa mafunzo kwa wakunga kuongeza weledi kwenye taaluma ya ukunga,” amesema.

Amesema kupitia mbio hizo, wanatarajia kuchochea uwekezaji na sera madhubuti zinazounga mkono taaluma ya ukunga.

“Wakunga ni nguzo muhimu ya uzazi salama, kwani wanaokoa maisha kila siku, hivyo, kuwezesha wakunga ni kuimarisha afya ya mama na mtoto na familia kwa ujumla,” amesema.

Mwakilishi wa Murugenzi wa Huduma za Ukunga Tanzania, Joyce Muna, amewataka wadau kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo Ili kufanikisha lengo la TAMA.

“Kila mmoja wetu hapa ajiandae kushiriki mbio hizo Ili kusaidia kuhamasisha shughuli za wakunga nchini, Kwa kutambua kuwa Wana jukumu kubwa,” amesema Joyce.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments