Tuesday, April 21, 2026
spot_img
HomeHabariSamia ang’ara Kongamano la Lishe

Samia ang’ara Kongamano la Lishe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Aprili 21, 2026 ameshiriki katika Kongamano la Kitaifa la Mama na Baba Lishe lililofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo, Rais Samia alivutia hisia za washiriki baada ya kuonekana akiwa amevalia vazi la kupikia, ishara ya kuunga mkono juhudi za kuimarisha lishe bora katika familia na jamii kwa ujumla.

Mbali na hilo, Rais Samia alitembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho, ambapo alipata maelezo kutoka kwa wadau kuhusu bidhaa na huduma zinazochangia kuboresha lishe nchini. Kongamano hilo limekusudia kuongeza uelewa kwa wazazi na walezi juu ya umuhimu wa lishe bora katika ukuaji na maendeleo ya watoto.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments