HomeBiasharaAirtel Money Tanzania kufanya maboresho katika Mfumo wake ili kuimarisha huduma bora

Airtel Money Tanzania kufanya maboresho katika Mfumo wake ili kuimarisha huduma bora

Airtel Money Tanzania kufanya maboresho katika Mfumo wake ili kuimarisha huduma bora na salama kwa wateja wake wote.

Dar es Salaam, Tanzania — 16 Oktoba 2026 — Airtel Money Tanzania imetangaza maboresho makubwa ya mfumo wake wa huduma za kifedha kwa njia ya simu, yaliyolenga kuongeza kasi, kuimarisha usalama, na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wateja.

Maboresho hayo ya mfumo wa huduma za Airtel Money yataanza kufanyika kuanzia siku ya Jumamosi, tarehe 17 Oktoba, saa 4:00 usiku, hadi yatakuwa yamekamilika na mfumo kurudi sawa saa 2:00 asubuhi, siku ya Jumapili, tarehe 18 Oktoba 2026. Baadhi ya huduma za Airtel Money hazitopatikana ndani ya kipindi cha maboresho.

Airtel Money Tanzania imejipanga vizuri kuhakikisha kwamba maboresho haya yanafanyika kwa muda mfupi ili kupunguza usumbufu kwa wateja, kwa msaada wowote, wateja wanaweza kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja kupitia namba 100 pekee.

Akizungumzia maboresho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Money Tanzania, Andrew Rugamba, alisema: “Wateja wetu ndio kiini cha kila kitu tunachofanya. Hivyo, maboresho haya yanalenga kuongeza kasi, uthabiti na usalama zaidi katika upatikanaji wa huduma kwa ajili ya wateja wetu.”

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments