HomeHabariWami/Ruvu yaweka kambi Mkuranga kutoa elimu ya uhifadhi wa maji

Wami/Ruvu yaweka kambi Mkuranga kutoa elimu ya uhifadhi wa maji

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeweka kambi maalumu katika Kijiji cha Kisemvule, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani, kwa lengo la kutoa elimu kuhusu uhifadhi wa rasilimali za maji, utunzaji wa mazingira na tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa.

Kambi hiyo, inayotarajiwa kudumu kwa wiki moja, pia inalenga kuwatambua wateja wapya na kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya maji, ulinzi wa vyanzo vya maji na umuhimu wa kutunza mito na maeneo ya hifadhi yake.

Kupitia kambi hiyo, wananchi wanahamasishwa kuepuka kutupa taka katika mito na mifereji ya maji, pamoja na kujenga au kufanya shughuli nyingine za kibinadamu ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji.

Elimu inayotolewa pia inalenga kuwajengea wananchi uelewa kuhusu tahadhari za kuchukua wakati wa mvua kubwa zinazoweza kusababisha mafuriko, ili kulinda maisha, mali na mazingira.

Wananchi wa Kisemvule na maeneo ya jirani wamekuwa wakitembelea banda la Bodi hiyo kupata elimu, kuuliza maswali na kuwasilisha changamoto zinazohusiana na rasilimali za maji. Ushirikiano huo unawapa fursa ya kupata ufafanuzi na kuelewa namna wanavyoweza kushiriki katika uhifadhi wa rasilimali hizo.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inaendelea kuhamasisha wananchi kushirikiana na Serikali katika kulinda vyanzo vya maji na kutunza mazingira, kwa lengo la kuhakikisha rasilimali hizo zinapatikana kwa matumizi ya sasa na vizazi vijavyo.

Wananchi wametakiwa kuzingatia elimu inayotolewa, kuchukua tahadhari dhidi ya hatari zinazoweza kuletwa na mvua kubwa na kushiriki kikamilifu katika kuzuia uharibifu wa mazingira.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments