- Mnara mpya wa mawasiliano wa 4G unatarajiwa kunufaisha takribani wakazi 2,000 wa Kata ya Mlingura na vijiji jirani.
MTWARA, Novemba 11, 2026. Airtel Tanzania inaendelea kusambaza zaidi miundombinu yake ya mawasiliano katika Wilaya ya Masasi, Mkoa wa Mtwara, kwa kusogeza huduma za uhakika za mtandao wa 4G karibu na jamii na kufungua fursa zaidi za kidigitali kwa wakulima, wafanyabiashara wadogo na kaya.
Hatua hiyo iliyofanyika kati ya Novemba 5 na Novemba 10, 2026, inajumuisha uzinduzi wa mnara mpya wa mawasiliano katika Kata ya Mlingura, eneo ambalo hapo awali lilikabiliwa na changamoto kubwa ya mawasiliano kutokana na kutokuwepo kwa huduma za mtandao wa uhakika.
Masasi ni miongoni mwa maeneo muhimu ya kilimo, ambapo shughuli za kiuchumi zinahusisha kilimo cha korosho na mihogo, uzalishaji wa matunda, uchakataji wa mazao na biashara. Kuimarika kwa mawasiliano kutawawezesha wakulima na wafanyabiashara wa mazao kupata taarifa muhimu, kuwasiliana na wanunuzi na wasambazaji pamoja na kutafuta masoko mapana zaidi ya bidhaa zao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mnara huo mpya wa mawasiliano Mlingura, Ben Mwantobe, Meneja Biashara wa Airtel Kanda ya Masasi, alisema upanuzi huo unaakisi dhamira ya kampuni ya kuwafikia wananchi ambao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za upatikanaji wa huduma za mawasiliano.
“Tumezindua mnara huu mpya kutokana na changamoto kubwa za mawasiliano ambazo wakazi wa eneo hili wamekuwa wakikabiliana nazo. Hapo awali, eneo hili halikuwa na mnara wa mawasiliano, hivyo tumeamua kuwasogezea huduma karibu na walipo. Dhamira yetu ni kuwafikia wananchi wenye changamoto za mawasiliano, kurahisisha mawasiliano na kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia Airtel Money,” alisema Mwantobe.
Kuimarika kwa mtandao kunarahisisha pia upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi. Kupitia mtandao bora, wakazi wanaweza kupata mawakala wa Airtel Money karibu na maeneo yao, hivyo kupunguza ulazima wa kusafiri hadi mjini Masasi kutoa fedha au kupata huduma nyingine za kifedha.
Wananchi pia watanufaika na upatikanaji bora wa intaneti ya simu, utakaowawezesha wakulima kupata taarifa za kilimo, utabiri wa hali ya hewa na bei za mazao sokoni. Wakati huohuo, wajasiriamali wataweza kutumia majukwaa ya kidijitali kutangaza bidhaa zao, kuwafikia wateja na kusimamia biashara zao kwa ufanisi zaidi.
Kwa wakazi wa maeneo hayo, kuimarika kwa mawasiliano kunaleta mabadiliko katika shughuli zao za kila siku.
Frumesa Simon, mkazi wa Kijiji cha Nambaya, alisema kuwa awali changamoto za mtandao ziliwalazimu wananchi kusafiri umbali mrefu kutafuta maeneo yenye mawasiliano ili waweze kupiga simu.
“Kabla ya kuwekwa kwa mnara wa Airtel, tulikuwa na changamoto kubwa sana ya mawasiliano. Wakati mwingine mtu alilazimika kutumia siku nzima kusafiri kwenda eneo lenye mtandao ili aweze kupiga simu. Tangu mnara huu uanze kutoa huduma, mawasiliano yameimarika kwa kiasi kikubwa na sasa tunapigiwa simu na kupatikana wakati wote,” alisema Simon.
Aliongeza kuwa upatikanaji wa huduma za Airtel Money umeimarika pia, huku wananchi wakipata urahisi zaidi wa kupata mawakala katika maeneo yao.
“Hapo awali, wananchi walilazimika kusafiri hadi mjini Masasi kupata huduma za Airtel Money na kutumia fedha za usafiri ambazo wangeweza kuzitumia kwa mahitaji mengine ya familia. Sasa mawakala wanapatikana karibu nasi, hivyo wananchi wanapata huduma kwa urahisi na kuokoa gharama za usafiri,” alisema.
Mkazi mwingine, Stella Michael, alieleza namna changamoto za mawasiliano zilivyokuwa zikiathiri upatikanaji wa taarifa muhimu, hususan zinazohusiana na shughuli za kikazi.
“Kabla ya kuboreka kwa mtandao, tulikuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa za mawasiliano. Mtandao ulikuwa unakatika mara kwa mara na wakati mwingine simu hazikuweza kupatikana. Hali hii ilisababisha hata taarifa muhimu za kikazi kuwafikia watu kwa kuchelewa, wakati mwingine baada ya vikao kuwa vimeanza,” alisema Michael.
Alisema kuwa hali imeimarika tangu kupatikana kwa huduma bora za mtandao, hivyo kuwawezesha wananchi kuwasiliana na kupata taarifa kwa wakati.
“Kwa sasa tunapatikana wakati wote tunapotafutwa. Tunaweza kuwasiliana, kutumia intaneti na simu zetu bila changamoto tulizokuwa tukizipata hapo awali. Mawasiliano ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku, kazi na upatikanaji wa taarifa. Tunaishukuru Airtel kwa kutusogezea huduma hizi karibu,” aliongeza.
Huduma bora za mawasiliano zinatarajiwa kuwanufaisha pia wakazi wa Kata ya Miyula kwa kurahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi. Upatikanaji wa mawasiliano na huduma za kifedha kwa urahisi zaidi utawawezesha wananchi kuwasiliana na ndugu, jamaa na washirika wao wa kibiashara pamoja na kupata huduma mbalimbali za kidijitali.
“Mawasiliano ya uhakika ni muhimu kwa maendeleo ya jamii yetu. Ujio wa mtandao wa Airtel umerahisisha wananchi kuwasiliana, kupata huduma za Airtel Money na kuwasiliana na ndugu pamoja na washirika wao wa kibiashara. Tunaishukuru Airtel kwa kutusogezea huduma hizi karibu na wananchi wetu,” alisema Dominic Milanzi, Diwani wa Kata ya Miyula.
Mwantobe alisema kuwa miundombinu hiyo mipya inatumia teknolojia ya 4G inayowawezesha wateja kupata intaneti yenye kasi zaidi na huduma bora za matumizi ya data.
“Kila mnara tunaouzindua unakuja na teknolojia ya 4G, inayowawezesha wateja kupata intaneti yenye kasi zaidi na huduma za uhakika za data. Hii inawapa wananchi fursa ya kuwasiliana na wapendwa wao, kutumia mitandao ya kijamii, kupata huduma za kifedha za kidijitali na kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana mtandaoni. Tutaendelea kupanua mtandao wetu ili kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuboresha huduma za mawasiliano nchini,” alisema.
Upanuzi wa mtandao Masasi ni sehemu ya mpango mpana wa Airtel Tanzania wa kuendelea kuimarisha huduma za mawasiliano katika mikoa ya kusini, ambao pia umejumuisha uzinduzi wa minara mipya katika maeneo ya Chiwata na Mbaka. Uzinduzi mwingine umepangwa kufanyika Mangaka, Wilaya ya Nanyumbu, na Wilaya ya Nachingwea, katika maeneo ya Ndomoni na Mnero Miembeni.
Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa idadi ya usajili wa huduma za intaneti nchini ilifikia milioni 62.79 kufikia Juni 2026, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.48 ndani ya robo mwaka. Matumizi ya data pia yaliongezeka kwa asilimia 11.65 na kufikia petabaiti 1,041, hali inayoonesha kuongezeka kwa umuhimu wa huduma za kidijitali katika shughuli za kila siku na kiuchumi.
Uwekezaji unaoendelea kufanywa na Airtel Tanzania katika miundombinu ya mawasiliano unaakisi dhamira ya kampuni ya kupanua upatikanaji wa huduma za kidijitali, kusaidia shughuli za kiuchumi katika jamii na kuunganisha wananchi wengi zaidi nje ya miji mikubwa.
Kwa kusogeza huduma za mawasiliano na kidijitali karibu na wakulima, wajasiriamali na kaya, Airtel inaendelea kutekeleza dhamira yake ya kuwaunganisha wananchi na kuwahudumia Airtel Kila Kona.




