HomeHabariWizara ya Viwanda yajipanga uongezaji thamani wa Chuma cha Liganga

Wizara ya Viwanda yajipanga uongezaji thamani wa Chuma cha Liganga

๐Ÿ“Œwatembelea kiwanda cha chuma cha sichuan kilichoko nchini China;

๐Ÿ“Œ Ziara ya ujumbe wa Tanzania nchini China inalenga kujifunza teknolojia za kisasa za uzalishaji wa chuma.

๐Ÿ“Œ Yalenga kuongeza fursa za uwekezaji kuongeza kasi utekelezaji wa Mradi wa Mchuchuma na Liganga.

๐Ÿ“Œ Kiwanda hicho ni kampuni tanzu ya Shudao Investment Group Co., Ltd., inayoshirikiana na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kupitia ubia katika utekelezaji wa Mradi wa Mchuchuma na Liganga nchini Tanzania.

CHINA: Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, akiambatana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Deodatus Mwanyika, wametembelea kiwanda cha kisasa cha uzalishaji wa bidhaa za miundombinu kwa kutumia malighafi ya chuma cha Sichuan Steel Structure Intelligent Manufacturing Co., Ltd. jijini Chengdu, China, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kikazi ya ujumbe wa Tanzania nchini humo.

Ziara hiyo inalenga kujifunza teknolojia za kisasa za uzalishaji wa chuma na kuchunguza fursa za uwekezaji na ushirikiano zitakazosaidia kuhakikisha utekelezaji wa Mradi Unganishi wa Makaa ya Mawe wa Mchuchuma na Chuma cha Liganga, ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha chuma, miundombinu ya nishati na makazi katika Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe unatekelezwa kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kiwanda cha Sichuan Steel Structure Intelligent Manufacturing Co., Ltd. kinajihusisha na usanifu na utengenezaji wa miundo mbalimbali ya chuma kwa kutumia teknolojia za kisasa za uzalishaji, kwa ajili ya matumizi ya ujenzi na miundombinu. Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha tani 160,000 za bidhaa za chuma kwa mwaka.

Kampuni hiyo ni kampuni tanzu ya Shudao Investment Group Co., Ltd., kampuni ya uwekezaji inayoshirikiana na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kupitia ubia katika utekelezaji wa Mradi wa Mchuchuma na Liganga nchini Tanzania.

Kutembelea kiwanda hicho ni sehemu ya jitihada za Tanzania kujifunza uzoefu, teknolojia na mifumo ya uzalishaji wa chuma kutoka kwa wawekezaji na kampuni zenye uzoefu katika sekta hiyo, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji na kuweka msingi wa maendeleo ya sekta ya chuma nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments