HomeBiasharaGambia yaja kujifunza mifumo ya udhibiti EWURA

Gambia yaja kujifunza mifumo ya udhibiti EWURA

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imekuwa kivutio kwa wadhibiti wa huduma kutoka Gambia, baada ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati, Maji, Mawasiliano na Usafiri (PURA) ya nchi hiyo kutembelea Tanzania kujifunza mifumo ya uendeshaji na usimamizi wa huduma zinazodhibitiwa.

Akizungumza wakati wa kuwapokea wajumbe hao, Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Profesa Mark Mwandosya, amesema mamlaka hiyo inaongozwa na misingi ya utaalamu, uwazi na uhuru wa maamuzi katika kutekeleza majukumu yake.

Amesema utendaji wa EWURA unazingatia maslahi ya watoa huduma, watumiaji na Serikali ili kuhakikisha huduma zinazodhibitiwa zinatolewa kwa ufanisi na kuleta matokeo yenye tija kwa jamii.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya PURA ya Gambia, Lucy Fye, amesema wamevutiwa na mifumo ya EWURA ya kushughulikia malalamiko ya wananchi, utoaji wa leseni na ufuatiliaji wa utendaji wa watoa huduma.

Ametaja maeneo mengine wanayotaka kujifunza kuwa ni mifumo ya utawala na uendeshaji wa taasisi hiyo pamoja na matumizi ya teknolojia katika utoaji wa leseni na vibali.

Amesema uzoefu wa EWURA katika maeneo hayo ni muhimu kwa PURA katika kuimarisha mifumo yake ya udhibiti na usimamizi wa huduma nchini Gambia.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments