HomeMichezoUchaguzi Mkuu Simba kufanyika Januari 30

Uchaguzi Mkuu Simba kufanyika Januari 30

Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Simba sasa utafanyika ifikapo Januari 30, mwakani hapa jijini, Dar es Salaam.

Awali uchaguzi huo ambao uliitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, ulipangwa kufanyika Januari 3, mwakani.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu, alisema uchaguzi huo unaitishwa kwa mujibu wa ibara ya 20 (6) na Ibara ya 22 (1) ya katiba ya klabu yao na utasimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Mangungu alisema uchaguzi huo utafanyika kwa kufuata katiba ya Simba ya mwaka 2018 (ambayo ilifanyiwa marekebisho Novemba, mwaka jana) na kusajiliwa Februari 18, mwaka huu.

“Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa Simba Sports Club wanataarifiwa kuwa mkutano mkuu wa kawaida utafanyika Jumamosi siku ya tarehe 30.01.2027 kuanzia saa 3:00 asubuhi,” ilisema sehemu ya taarifa ya Mangungu.

Mwenyekiti huyo ametangaza siku mpya ya kufanyika uchaguzi kama alivyoelekezwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyoko chini ya Kiomoni Kibamba.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments