Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga, ambaye alikuwa akitibiwa nchini India, amefariki baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo.
Alikimbizwa hospitalini ambako alitangazwa kufariki mwendo wa saa 9:52 asubuhi (saa za India), kulingana na Msemaji wa hospitali hiyo.
Kulingana na ripoti kutoka India, binti yake na jamaa walikuwa pamoja naye.
Odinga ambaye alikuwa na umri wa miaka 80 ni Mwanasiasa Mashuhuri wa Kenya ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuanzia 2008-2013.




