HomeHabariMradi wa TAZA kuchochea Viwanda, Ajira Na Uwekezaji

Mradi wa TAZA kuchochea Viwanda, Ajira Na Uwekezaji

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema Mradi wa Kuunganisha Gridi za Umeme za Tanzania na Zambia (TAZA) utaimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuongeza uzalishaji na kufungua fursa mpya za uwekezaji katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Amesema mradi huo utasaidia kuchochea shughuli za kiuchumi, hususan uchakataji wa mazao ya kilimo, uanzishaji wa viwanda na upanuzi wa biashara, hatua zitakazoongeza thamani ya mazao, kukuza kipato cha wananchi na kutengeneza ajira.

Ndejembi ameyasema hayo leo, Oktoba 15, 2026, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, ikiwemo ujenzi wa vituo vya kupokea na kupoza umeme vya Malangali mkoani Rukwa na Nkangamo mkoani Songwe.

Akiwa katika Kituo cha Malangali, Ndejembi amesema Mkoa wa Rukwa umekuwa ukikabiliwa na upungufu wa umeme unaoathiri uzalishaji na ukuaji wa uchumi. Kwa sasa, mkoa huo hupokea takribani megawati 16 za umeme, wakati mahitaji yake yakifikia megawati 30.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments