Saturday, March 7, 2026
spot_img
HomeBiasharaKCB Bank yaandaa Iftar Zanzibar

KCB Bank yaandaa Iftar Zanzibar

KCB Bank Tanzania imeandaa hafla maalumu ya Iftar katika Golden Tulip Zanzibar Resort kwa lengo la kuimarisha mshikamano na wateja pamoja na wadau wa maendeleo katika msimu wa mwezi mtukufu wa Ramadan.

Hafla hiyo iliyofanyika Zanzibar ilihudhuriwa na viongozi wa serikali, viongozi wa dini pamoja na wafanyabiashara, huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Juma Malik Akil.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Shariah ya KCB Bank Tanzania, Sheikh Khamis Mataka, alisisitiza umuhimu wa kufanya biashara kwa uadilifu, uwazi na misingi ya kumcha Mungu, ambayo ni nguzo kuu ya huduma za Sahl Banking.

Alisema kupitia huduma hiyo, wateja wanapata fursa mbalimbali za kifedha zikiwemo Murabaha (ufadhili wa faida badala ya riba), Qard Hasan (mikopo ya muda mfupi isiyo na riba), pamoja na akaunti maalum za Hijja na akiba.

Mataka aliongeza kuwa benki hiyo pia inaendesha programu ya uwezeshaji vijana inayojulikana kama 2Jiajiri inayotoa mafunzo ya ujasiriamali na ujuzi wa kiuchumi kwa vijana. Aidha, benki hiyo imekuwa ikisaidia nyumba za watoto yatima visiwani Zanzibar.

Kwa upande wake, Waziri Juma Malik Akil aliipongeza KCB Bank kwa jukumu lake la kuwa daraja kati ya mfumo wa kibenki wa kawaida na mahitaji ya kimaadili ya jamii ya Zanzibar.

Alihimiza benki hiyo kuendelea kubuni bidhaa za kifedha zinazoendana na dira ya serikali ya kujenga uchumi wa kidijitali na jumuishi.

Hafla hiyo ya Iftar imelenga pia kuimarisha mahusiano kati ya KCB Bank Tanzania na jamii, hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments