HomeBiasharaMinyoosho Inaendelea na My Airtel App: Washindi wengi zaidi, Zawadi nyingi zaidi...

Minyoosho Inaendelea na My Airtel App: Washindi wengi zaidi, Zawadi nyingi zaidi kupitia My Airtel Money App

●      Kila muamala unaofanyika kupitia My Airtel App unakupa nafasi ya kuzungusha gurudumu na kushinda.

●      Airtel yaendelea kurahisisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali kwa usalama zaidi huku ikiwazawadia wateja wanaofanya miamala ya kila siku.

DAR ES SALAAM: Airtel Money imezindua rasmi kampeni ya “Minyoosho Inaendelea na My Airtel App” yenye lengo la kuwahamasisha wateja kutumia huduma za kifedha kidijitali kupitia programu hiyo huku wakipata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali.

Kampeni hiyo ya miezi mitatu inawalenga wateja wote wanaotumia My Airtel App kufanya miamala ya kila siku, ambapo baada ya kukamilisha muamala hupata fursa ya kuzungusha gurudumu la kidijitali (Spin & Win) na kujishindia zawadi papo hapo.

Kupitia kampeni hiyo, wateja wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo pikipiki, runinga, simu janja, fedha taslimu pamoja na zawadi nyingine zinazotolewa moja kwa moja baada ya kushiriki.

Wateja wanapata nafasi ya kushinda kwa kufanya miamala mbalimbali kupitia My Airtel App, ikiwemo kutuma fedha, kufanya malipo, kununua muda wa maongezi na vifurushi vya intaneti, kulipa bili, kufanya miamala ya kimataifa pamoja na kulipia huduma ya Home Broadband.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, Andrew Rugamba, amesema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya kampuni hiyo ya kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za kifedha kidijitali kwa urahisi na usalama.

“Kupitia kampeni yetu ya Minyoosho Inaendelea na My Airtel App, tunataka kuona wateja wetu wanahamasika kutumia Airtel App kufanya miamala yao ya kila siku. Kila muamala utampa mteja nafasi ya kushinda zawadi papo hapo,” amesema Rugamba.

Amesema Airtel ni miongoni mwa kampuni zilizoanzisha matumizi ya mfumo wa michezo ya zawadi katika huduma za kifedha kidijitali (gamification) kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wananchi katika uchumi wa kidijitali.

Rugamba amesema lengo la kampeni hiyo si kutoa zawadi pekee, bali pia kuwahamasisha Watanzania kutumia huduma za kifedha kidijitali na kuchangia ukuaji wa uchumi jumuishi.

Kampeni ya “Minyoosho Inaendelea na My Airtel App” inaendana na dira ya “Airtel Kila Kona” inayolenga kusogeza huduma za kidijitali karibu na Watanzania wote mijini na vijijini kupitia teknolojia rahisi na inayopatikana kwa urahisi.

Airtel atoa tahadhari dhidi ya utapeli

Katika kipindi cha kampeni hiyo, Airtel Money imewakumbusha wateja kuwa makini dhidi ya vitendo vya udanganyifu na utapeli wa kifedha mitandaoni.

Airtel imesema washindi watawasiliana na kampuni hiyo kupitia namba rasmi ya huduma kwa wateja 100 pekee na kupokea ujumbe rasmi wa SMS wanaposhinda.

Wateja wametakiwa kutotoa taarifa zao binafsi, ikiwemo namba ya siri ya Airtel Money (PIN), namba za uthibitisho (OTP) au nywila kwa mtu yeyote anayejitambulisha kuwa mfanyakazi wa Airtel kupitia namba zisizo rasmi.

Kampuni hiyo imewahimiza wateja kupakua My Airtel App, kufanya miamala na kushiriki katika kampeni hiyo ili kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali wakati wowote na mahali popote.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments