Wednesday, April 1, 2026
spot_img
HomeBiasharaBei petroli, dizeli zapanda kwa asilimia 33

Bei petroli, dizeli zapanda kwa asilimia 33

Bei za petroli na dizeli nchini zimepanda kwa zaidi ya asilimia 33 kwa mwezi Aprili 2026, kufuatia ongezeko la gharama katika soko la dunia, kwa mujibu wa EWURA.

Takwimu zinaonyesha kuwa bei ya petroli katika jiji la Dar es Salaam imeongezeka kutoka Sh. 2,864 kwa lita mwezi Machi hadi Sh3,820 mwezi Aprili, sawa na ongezeko la takribani Sh. 956 kwa lita. Bei ya dizeli imepanda kutoka Sh2,858 hadi Sh. 3,806, ikiwa ni ongezeko la Sh. 948 kwa lita.

Kwa upande wa mafuta ya taa, bei imeongezeka hadi Sh. 3,684 kutoka Sh. 2,932, sawa na ongezeko la takribani Sh. 752 kwa lita.

EWURA imesema kupanda kwa bei kunatokana na athari za mgogoro wa Mashariki ya Kati uliosababisha kuongezeka kwa gharama za mafuta katika soko la dunia, pamoja na kupanda kwa gharama za usafirishaji na bima ya mizigo.

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa hatari katika njia muhimu za usafirishaji wa mafuta, ikiwemo Lango la Hormuz, zimechangia ongezeko la gharama za uagizaji wa mafuta.

‎Pamoja na ongezeko hilo, EWURA imesisitiza kuwa upatikanaji wa mafuta nchini unaendelea kuwa wa kuridhisha, huku ikiwataka wafanyabiashara kuzingatia bei kikomo zilizotangazwa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments