HomeBiasharaWananchi Rufiji kunufaika na elimu ya biashara ya Kaboni

Wananchi Rufiji kunufaika na elimu ya biashara ya Kaboni

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamadi Yussuf Massauni amekielekeza Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) mkoani Morogoro kutoa elimu ya Biashara ya Kaboni kwa wananchi wa Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani. 

Masauni ameyasema hayo wakati akiwa wilayani humo kwenye ziaraa ya kikazi, Julai 21, 2026 wakati akieleza fursa na faida za uhifadhi wa mazingira ukiwemo utunzaji wa misitu. 

Amesema wakazi wa Rufiji wanapaswa kutumia fursa katika biasharara ya kaboni kujikwamua kiuchumi na Ofisi ya Makamu wa ipo tayari kutuma wataalam kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi waliokuwa tayari kufanya biashara hiyo.

 “Sina uhakika kama mmeshaanza ila kama bado mnaweza kuanza ili mfike mbali zaidi, miradi ya utunzaji wa Mazingira ikiwemo migomba, mikorosho ni biashara nzuri kwenye kaboni, watumieni wataalamu wawape muongozo kuongeza kipato ili kutumia fursa hii,” amesema Waziri Masauni.

 Waziri Masauni pia amesema mabadikiko tabia nchi ni chanzo cha biashara hiyo ndio na kwamba kupitia mkataba wa Paris walikubaliana nchi zenye rasilimiali katika kupunguza hewa ya ukawa zilipwe.

 “Utakuta misitu imezagaa zagaa watu wanakata miti ovyo bila kukua hii ni biashara inaweza kuwakwamua kiuchumi hata mtu mmoja mmoja au vikundi”, amesema.

 “Lengo letu tunataka kila fursa inayogusa fursa kwenye biashara ya kaboni inafumika ipasavyo wanarufiji, mkitumia fursa hii vizuri itawasaidi wengi wenu kwani walioanza tayari wanavuna matunda,”,” amesema.

 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema mkoa huo kwasasa unaongoza katika mambo mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato, ujenzi wa viwanda na ufaulu katika sekta ya elimu.

 Kunenge amesema uwekezaji mkubwa umefanyika ikiwemo kiwanda cha sukari ambacho kimejengwa Rufiji na Viwanda vingine ambavyo vinakuza ajira kwa mji huo.

 Amesema muelekeo wa Serikali kuelekea katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo 2050 ni kuwa na ajira zaidi na kuongeza mapato ya nchi ambapo kila mmoja itamgusa katika eneo lake.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Luten Kanal Frederick Komba amesema Serikali ya wilaya hiyo inaendelea kusimamia shughuli za maendeleo na makusanyo ya mapato huku wakijikita kulinda vyanzo vya mapato vilivyopo.

 Amesema pia wanaendelea kutekeleza maagizo ya kupanda miti 1,500 kila mwaka ikiwemo miti ya matunda kwenye maeneo mbalimbali ya Taasisi na makazi ya wananchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments