Klabu ya Simba SC imethibitisha kuendelea kuwa na mshambuliaji Seleman Mwalimu ‘Gomez’ baada ya kuongeza mkataba wake wa mkopo kwa mwaka mmoja zaidi kutoka Wydad Casablanca ya Morocco kuelekea msimu wa 2026/27.
Gomez, aliyefunga mabao tisa katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/26, amepewa nafasi ya kuendelea kuitumikia Simba baada ya kiwango chake kizuri kuwavutia viongozi na benchi la ufundi. Simba imesema hatua hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kuimarisha kikosi kwa mashindano ya ndani na kimataifa msimu ujao.






