HomeElimu‎NACTVET yaonesha mafanikio ya elimu ya amali

‎NACTVET yaonesha mafanikio ya elimu ya amali

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linaendelea kuonesha mafanikio ya utekelezaji wa elimu ya amali katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo wanafunzi kutoka shule za sekondari zenye mkondo wa amali wanawasilisha kwa vitendo ujuzi na ubunifu walioupata kupitia masomo hayo.

‎Katika banda la NACTVET, wageni wanapata fursa ya kushuhudia bidhaa na kazi mbalimbali zilizobuniwa na wanafunzi pamoja na kupata ushuhuda wao kuhusu namna elimu ya amali ilivyowawezesha kupata ujuzi wa kujitegemea na kujiandaa kwa ajira na kujiajiri.



‎Mbali na maonesho hayo, wataalamu wa NACTVET wanatoa elimu kuhusu nafasi ya Baraza katika kusimamia ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini. Wananchi pia wanapata taarifa kuhusu fursa za masomo zinazopatikana katika vyuo vinavyosimamiwa na Baraza, taratibu za udahili pamoja na huduma mbalimbali zikiwemo Namba ya Utambuzi na Tuzo (AVN) na utoaji wa hati za matokeo.

‎Ushiriki wa NACTVET katika maonesho hayo unaendelea kutoa nafasi kwa wananchi kujifunza kuhusu mchango wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi katika kukuza ujuzi, ubunifu, ajira na maendeleo ya uchumi wa Taifa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments