“Leo ni siku ya Mashujaa. Nchi yetu ina mashujaa wengi. Leo naomba niwaongelee mashujaa wa vita ya Kagera.
Ninatoa rai kwa Serikali kuharakisha mchakato wa kuwaenzi mashujaa wa vita ya Kagera kwa kuwapolipa posho.
Mwaka wa Fedha uliopita (2025/2026) Serikali iliahidi wataanza kulipwa posho, hawkaulipwa.
Mwaka huu wa fedha (2026/2027) Serikali imeahidi Wataanza kulipwa mapema kwa sababu uhakiki umekamilika, hawajalipwa.
Ni muhimu Serikali iwakumbuke mashujaa hawa kwa kuwalipa mapema iwezekanavyo”- Ado Shaibu Ado, Mbunge wa Tunduru Kaskazini na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo




