HomeMichezoTAMFA kuenzi Nyerere kwa kukuza michezo na vipaji

TAMFA kuenzi Nyerere kwa kukuza michezo na vipaji

Chama cha Mini Football Tanzania (TAMFA) kinatarajia kutumia bonanza la michezo litakalofanyika katika viwanja vya Muhimbili, Dar es Salaam, kuibua na kukuza vipaji vya vijana pamoja na kuhamasisha maendeleo ya mchezo huo nchini.

Bonanza hilo litaandaliwa katika maadhimisho ya kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutambua mchango wake katika maendeleo ya taifa.

Akizungumza Dar es Salaam, Rais wa TAMFA, Deusdedit Mushi, amesema bonanza hilo linalenga kutoa fursa kwa vijana kuonesha vipaji vyao na kupata nafasi ya kuendelezwa kupitia mchezo wa Mini Football.

“Tumeamua kuandaa bonanza hilo la kimichezo lenye lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana kupitia mchezo huu na kuenzi yale yote yaliyofanywa na Mwalimu Nyerere,” amesema Mushi.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Benki ya MCB, Ana Mgaya, amesema benki hiyo imeamua kushirikiana na TAMFA kama mdhamini mkuu wa bonanza hilo ili kusaidia kuibua vipaji na kuwaunganisha watu kupitia michezo.

Naye kocha wa Mini Football, Seif Jamal, amesema atatumia bonanza hilo kutathmini uwezo wa wachezaji mmoja mmoja kwa lengo la kubaini vipaji vinavyoweza kuendelezwa.

Bonanza hilo linatarajiwa kuwa fursa kwa vijana kuonesha uwezo wao na kuongeza mwamko wa mchezo wa Mini Football nchini.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments