HomeBiashara‎TVLA yatoa elimu ya huduma za mifugo maadhimisho ya miaka 50

‎TVLA yatoa elimu ya huduma za mifugo maadhimisho ya miaka 50

Na Daudi Nyingo, Morogoro

‎Elimu hiyo imetolewa Novemba 25, 2026, wakati wa maonesho ya kuadhimisha miaka 50 ya mafunzo ya tiba ya wanyama nchini, yaliyoandaliwa na SUA kwa kushirikiana na Chama cha Madaktari wa Mifugo Tanzania (TVA).

Madaktari wa mifugo, wanafunzi na wadau wa sekta hiyo wamepatiwa elimu kuhusu uchunguzi wa magonjwa ya wanyama, chanjo na uhakiki wa ubora wa vyakula vya mifugo kupitia maonesho ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) yanayofanyika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro.

‎Wataalamu wa TVLA walioongozwa na Dk. Jumanne Jumbe, Dk. Scholastica P. Doto na Paulo Joseph wamewafafanulia wageni majukumu ya wakala huo, huduma zinazotolewa kupitia maabara na vituo vyake, pamoja na taratibu za kuzipata.

‎Miongoni mwa huduma zilizoelezewa ni uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya wanyama, uzalishaji na upatikanaji wa chanjo za mifugo, pamoja na uhakiki wa ubora wa vyakula vya mifugo.

‎Wageni pia wamepata elimu kuhusu uhakiki na usajili wa viuatilifu vya mifugo na majukumu ya TVLA katika kusaidia kuimarisha afya na uzalishaji wa mifugo nchini.

‎Maonesho hayo yanaendelea hadi Novemba 27, 2026, yakitoa fursa kwa madaktari wa mifugo, wanafunzi na wadau wengine kutembelea banda la TVLA na kupata maelezo ya kitaalamu kuhusu bidhaa na huduma zake.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments